Hapa ndipo unapoweza kupata majibu ya baadhi ya maswali tunayoulizwa sana kuhusu faragha, kama vile Data ni nini? Angalia pia Sera ya Faragha iwapo ungependa kupata maelezo zaidi.
Faragha yako kwenye Google
Mahali ulipo
Je, Google hujua mahali nilipo?
Wakati wowote unapotumia intaneti, programu na tovuti zinaweza kukadiria mahali ulipo na Google pia inaweza kufanya hivyo. Google inaweza pia kujua eneo mahususi ulipo, kulingana na mipangilio ya kifaa chako. (Angalia sehemu ya Je, mahali nilipo pana usahihi wa kiasi gani?)
Unapotafuta kwenye Google, kama vile ukitumia huduma ya Tafuta, Ramani au Mratibu wa Google, maelezo ya mahali kwa wakati huo hutumiwa ili kukupa matokeo yanayokufaa zaidi. Kwa mfano, ukitafuta mikahawa, matokeo yanayokufaa zaidi yanaweza kuwa mikahawa iliyo karibu na mahali ulipo.
Angalia sehemu ya Unavyoweza kudhibiti maelezo ya mahali ulipo
Ninawezaje kuwasha au kuzima mipangilio ya mahali?
Ukitafuta kwenye Google, Google itakadiria eneo la jumla ambako unatafutia. Sawa na programu au tovuti yoyote unayotumia inayounganishwa kwenye Intaneti, Google inaweza kukadiria mahali ulipo kulingana na anwani ya IP ya kifaa chako. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Google hujuaje mahali nilipo?.
Ili uchague iwapo ungependa kutuma maelezo ya eneo mahususi ulipo unapotumia Google, unaweza kuwasha au kuzima ruhusa za mahali kwenye programu au tovuti mahususi na kwenye kifaa chako.
Ukiweka anwani yako ya nyumbani au ya kazini na Google ikadirie kwamba upo nyumbani au kazini, basi anwani hiyo mahususi itatumiwa kwa ajili ya utafutaji wako.
Je, mahali nilipo ni mahususi kwa kiasi gani?
Eneo la jumla uliko
Ukitafuta kwenye Google, Google itakadiria eneo la jumla ambako unatafutia. Kwa njia hii, Google inaweza kukupa matokeo yanayofaa na kuimarisha usalama wa akaunti yako kwa kutambua shughuli zisizo za kawaida, kama vile tukio la kuingia katika akaunti kwenye jiji tofauti.
Eneo la jumla ni kubwa kuliko kilomita tatu mraba na lina angalau watumiaji 1,000 ili eneo la jumla ambako unatafutia lisikutambulishe. Hali hii husaidia kulinda faragha yako.
Eneo mahususi ulipo
Ukiiruhusu, Google inaweza kutumia maelezo ya eneo mahususi ulipo. Kwa mfano, Google inahitaji maelezo ya eneo mahususi ulipo ili ikupe matokeo yanayokufaa zaidi unapotafuta vitu kama vile “aiskrimu karibu nami” au maelekezo ya kutembea hatua kwa hatua kuelekea dukani.
Eneo mahususi linamaanisha mahali ulipo haswa, kama vile anwani maalum.
Google hujuaje mahali nilipo?
Maelezo yako ya mahali hutokana na vyanzo tofauti vinavyotumiwa kwa pamoja kukadiria mahali ulipo.
Anwani ya IP ya kifaa chako
Anwani za IP kimsingi hutegemea maeneo ya kijiografia, kama ilivyo misimbo ya maeneo ya nambari za simu. Hii inamaanisha kwamba programu au tovuti yoyote unayotumia, ikiwa ni pamoja na google.com, inaweza kukadiria eneo la jumla uliko kutokana na anwani yako ya IP. Anwani ya IP ya kifaa chako hukabidhiwa kifaa chako na Mtoa Huduma za Intaneti na inahitajika ili uweze kutumia intaneti.
Mahali kifaa chako kilipo
Ukiipa programu au tovuti ya Google ruhusa ya kutumia maelezo ya mahali kifaa chako kilipo, maelezo hayo yanaweza kutumika kusaidia kuelewa mahali ulipo. Takriban vifaa vyote vina mipangilio ya mahali iliyojumuishwa kwenye mfumo wa uendeshaji, kwa kawaida huwa katika mipangilio.
Shughuli zako kwenye Google
Google inaweza kukadiria eneo la jumla uliko, kutokana na utafutaji wako wa awali kwenye Google. Kwa mfano, ikiwa una mazoea ya kutafuta maeneo ya piza Mumbai, inawezekana ungependa kuona matokeo yaliyo katika eneo la Mumbai.
Maeneo uliyowekea lebo
Ukiweka anwani yako ya nyumbani au ya kazini, Google inaweza kuitumia kukadiria mahali ulipo. Kwa mfano, iwapo umeweka anwani yako ya nyumbani, anwani ya IP, shughuli zako za awali au vyanzo vingine vya maelezo ya mahali vikidokeza kwamba huenda uko karibu na nyumbani, basi tutatumia eneo la nyumbani kwako kukadiria mahali ulipo.
Ni nani anaweza kuona mahali nilipo?
Uamuzi ni wako. Ukitumia Kipengele cha Google cha Kushiriki Mahali Ulipo, unaweza kushiriki mahali ulipo katika muda halisi na marafiki na familia kwenye programu na tovuti mbalimbali za Google.
Angalia iwapo unashiriki maelezo ya mahali ulipo
Kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kimezimwa kwa chaguomsingi. Iwapo ungependa kushiriki maelezo ya mahali ulipo katika muda halisi, unahitaji kuchagua na kuthibitisha unayetaka kushiriki naye na kwa muda gani. Unaweza kuacha kushiriki mahali ulipo wakati wowote.
Angalia sehemu ya Kushiriki na wengine mahali ulipo katika muda halisi.
Kushiriki kwenye Google
Watu wengine wanaweza kuona maelezo gani ninaposhiriki kwenye Google?
Maelezo yako yanayoweza kuonekana kwa watu wengine kwenye programu na tovuti za Google yanategemea taarifa unazoshiriki na jinsi unavyoyashiriki:
Kushiriki hadharani
Ukichangia kwenye programu kama vile Ramani za Google, watu wengine wanaweza kuona jina na picha yako. Kwa mfano, ukikadiria duka la aiskrimu ulipendalo, watu wengine wanaweza kuona ukadiriaji wako, jina na picha yako wakiangalia maelezo ya duka hilo kwenye Ramani za Google.
Kushiriki kwa faragha
Ukishiriki na wengine vitu kama vile picha, video na hati, jina na picha yako huonekana kwa mtu unayemtumia.
Fikiria kwa umakini kabla ya kushiriki na wengine na uelewe kiwango cha uwezo wa kufikia unachowapa. Kwa mfano, unaposhiriki uwezo wa kufikia vitu kama vile folda katika Hifadhi ya Google au albamu katika huduma ya Picha kwenye Google, huenda watu wakaendelea kuwa na uwezo wa kufikia kadri unavyoongeza maudhui mapya.
Ni nani anayeweza kuona vitu ninavyoshiriki, kama vile picha, video na hati?
Unaweza kuchagua kushiriki maudhui mahususi na watu wengine katika programu na tovuti za Google unazotumia.
Usisahau kwamba ukishiriki, watu wengine wanaweza kushiriki tena, hata katika programu na tovuti zilizo nje ya Google.
Unaweza kufuta maudhui yako mwenyewe kwenye akaunti yako wakati wowote, lakini hatua hii haifuti nakala ambazo tayari umezishiriki.
Kuwa makini kuhusu maudhui unayoyashiriki na ushiriki tu na watu unaowaamini.
Je, Google hushiriki taarifa zangu binafsi na wengine?
Hatushiriki taarifa zako binafsi na kampuni, mashirika au watu binafsi nje ya Google isipokuwa katika hali chache kama vile tunapohitajika na sheria kufanya hivyo.
Ikiwa una Akaunti ya Google kupitia shule yako (akaunti ya Google Workspace for Education), msimamizi wa shule anayedhibiti akaunti yako atakuwa na uwezo wa kufikia taarifa zako.
Uwezo wa kufikia wa wasimamizi wa shule
Huenda msimamizi wa shule yako akaweza kufikia taarifa zifuatazo katika akaunti yako ya Google Workspace for Education:
- Kufikia na kuhifadhi taarifa zilizowekwa katika akaunti yako, kama vile barua pepe zako
- Kuona takwimu kuhusu akaunti yako, kama vile idadi ya programu unazosakinisha
- Kubadilisha nenosiri la akaunti yako
- Kusimamisha au kukomesha idhini yako ya kufikia akaunti
- Kupokea taarifa za akaunti yako ili kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria, au ombi husika la serikali linaloweza kutekelezwa
- Kuzuia uwezo wako wa kufuta au kubadilisha taarifa au mipangilio yako ya faragha
Sababu za Google kushiriki taarifa zako
Unapotupatia ruhusa
Kwa mfano, ukitumia Mratibu wa Google kuagiza piza, tutaomba ruhusa yako kabla ya kushiriki jina au nambari yako ya simu na mkahawa husika. Angalia sehemu ya Jinsi ambavyo Google hukusaidia kushiriki data kwa usalama na programu na huduma za wengine.
Na wasimamizi wa vikoa, kama ilivyoelezwa hapo juu.
Kwa ajili ya uchakataji wa nje: Tunatoa taarifa binafsi kwa kampuni tunazofanya kazi nazo ili ziweze kuchakata data kulingana na maagizo tunayozipa. Kwa mfano, tunatumia kampuni za nje ili zitusaidie kutoa usaidizi kwa wateja na tunalazimika kushiriki taarifa binafsi na kampuni hizo ili ziweze kujibu maswali ya watumiaji.
Kwa sababu za kisheria
Tutashiriki taarifa binafsi nje ya Google ikiwa tunaaamini kuwa kufanya hivyo ni muhimu kwa:
- Kutimiza sheria, kanuni, mchakato wa kisheria, au ombi husika la serikali linaloweza kutekelezwa
- Kutekeleza Sheria na Masharti husika, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa ukiukaji unaoweza kutokea.
- Kugundua, kuzuia au kushughulikia masuala ya ulaghai, usalama au ufundi.
- Kulinda dhidi ya ukiukaji wa haki, madhara kwa mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma kama inavyohitajika au kuruhusiwa na sheria.
Data na kuweka mapendeleo
Google hukusanya data gani kunihusu?
Unapotumia programu na tovuti za Google, tunakusanya taarifa tunazohitaji ili kukupa programu na tovuti hizo, kuzifanya zikufae zaidi na kwa sababu nyingine kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya Kwa nini Guugle hukusanya data?.
Kwenye mipangilio yako, unaweza kudhibiti data tunayokusanya na jinsi data hiyo inavyotumiwa. Kwa mfano, iwapo hutaki tuhifadhi Historia yako ya YouTube kwenye Akaunti yako ya Google, unaweza kuzima kipengele cha Historia ya YouTube. Angalia sehemu ya Ninawezaje kuamua data inayohifadhiwa na Google?
Data ni nini?
Taarifa zako binafsi ni pamoja na vitu unavyotupa vinavyokutambulisha, kama vile jina lako au anwani yako ya barua pepe. Pia ni pamoja na data nyingine ambayo Google inaweza kuhusisha nawe, kama vile taarifa tunazohusisha nawe katika Akaunti yako ya Google.
Taarifa zako binafsi zinajumuisha vitu vya aina mbili:
Vitu unavyotoa au kuunda
Unapofungua Akaunti ya Google, unatupa taarifa binafsi kama vile jina lako na nenosiri.
Unaweza pia kuhifadhi maudhui unayounda, unayopakia, au kupokea kutoka kwa watu wengine, kama vile ujumbe wa barua pepe na picha.
Mambo unayoyafanya kwenye Google
Tunakusanya taarifa kuhusu shughuli zako katika huduma zetu, taarifa hizo zinaweza kujumuisha vitu kama vile hoja unazozitafuta na video unazotazama, watu unaowasiliana nao au unaoshiriki maudhui nao na historia yako ya kuvinjari kwenye Chrome ili tuweze kuboresha hali yako ya utumiaji.
Tunakusanya taarifa kuhusu programu, vivinjari na vifaa unavyotumia kufikia huduma za Google. Kufanya hivyo hutusaidia kutoa vipengele kama vile kupunguza ung'avu wa skrini yako ikiwa chaji ya betri yako inakaribia kuisha.
Sisi huchakata maelezo ya mahali ulipo, kwa mfano unapotumia vipengele kama vile maelekezo ya kutembea hatua baada ya hatua. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Mahali.
Kwa nini Google hukusanya data?
Tunakusanya taarifa tunazohitaji ili kutoa huduma zetu, kuzifanya zikufae zaidi na kwa sababu nyingine kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya "Jinsi tunavyotumia data".
Kwa mfano, huduma ya Ramani za Google inaweza kukusaidia kufika unakokwenda kwa kuepuka msongamano wa magari kwa sababu inakusanya maelezo kuhusu mahali ulipo (data yako) na data ya umma (ramani na maelezo kuhusu maeneo ya umma).
Jinsi tunavyotumia data
Kutoa huduma zetu
Tunatumia data kutoa huduma zetu, kama vile kuchakata hoja unazotafuta ili kukupa matokeo.
Kudumisha na kuboresha huduma zetu
Data hutusaidia kudumisha na kuboresha huduma zetu. Kwa mfano, tunaweza kufuatilia hitilafu. Kutambua hoja za utafutaji ambazo huendelezwa visivyo mara kwa mara hutusaidia kuboresha vipengele vya kikagua tahajia vinavyotumika katika huduma zetu mbalimbali.
Kuunda huduma mpya
Data hutusaidia kuunda huduma mpya. Kwa mfano, baada ya kuelewa jinsi watu walivyopanga picha zao katika programu ya Picasa ambayo ilikuwa programu ya kwanza ya picha ya Google, tuliweza kubuni na kuzindua huduma ya Picha kwenye Google.
Kutoa huduma zilizowekwa mapendeleo, ikiwa ni pamoja na maudhui na matangazo
Tunatumia data kutoa maudhui yaliyowekwa mapendeleo, kwa mfano, mapendekezo ya video ambazo huenda ukazipenda. Kulingana na mipangilio uliyoweka na umri wako, huenda tukakuonyesha matangazo yaliyowekwa mapendeleo kwa kutegemea mambo yanayokuvutia.
Kupima utendaji
Pia tunatumia data kupima utendaji na kuelewa jinsi huduma zetu zinavyotumiwa
Kuwasiliana nawe
Huenda tukatumia anwani yako ya barua pepe kukutumia arifa tukitambua shughuli ya kutiliwa shaka
Kulinda Google, watumiaji wetu na umma
Tunatumia data kuimarisha usalama wa watu mtandaoni, kama vile kutambua na kuzuia ulaghai
Google hutumiaje data kuweka mapendeleo ya vitu?
“Kuweka mapendeleo” kunahusu kutumia taarifa tunazokusanya kufanya programu na tovuti zetu zikufae, kwa mfano:
- Mapendekezo ya video ambazo huenda ukazipenda
- Vidokezo vya usalama vilivyotokana na jinsi unavyotumia programu na tovuti za Google (angalia sehemu ya Ukaguzi wa Usalama)
Pia tunatumia data kuweka mapendeleo ya matangazo isipokuwa katika hali ambapo mipangilio hiyo imezimwa au kwa watu wenye umri fulani.
Je, Google huwekea mapendeleo matangazo ninayoyaona?
Sisi hujaribu kufanya matangazo tunayokuonyesha yawe muhimu iwezekanavyo. Lakini hatuweki mapendeleo ya matangazo kwa watu wenye umri fulani au kwa watu waliozima kipengele cha Kuweka mapendeleo ya matangazo.
Bado tunaweza kufanya matangazo yawe muhimu hata bila kuyawekea mapendeleo. Kwa mfano, ikiwa unatazama ukurasa wenye matokeo ya “viatu vipya,” huenda ukaona tangazo kutoka kwa kampuni ya viatu vya raba. Tangazo linaweza kutegemea vigezo vya jumla kama vile wakati, eneo la jumla uliko na maudhui ya ukurasa unaoangalia.
Uamuzi ni wako
Ninawezaje kuamua data inayohifadhiwa na Google kwenye akaunti yangu?
Unapotumia huduma ya Google, kama vile huduma ya Picha kwenye Google, kuna mipangilio inayokuwezesha kuamua mambo kama vile iwapo ungependa kuhifadhi nakala za picha zako na kuzisawazisha.
Pia kuna mipangilio inayokusaidia kufanya hali yako ya utumiaji wa programu na tovuti mbalimbali za Google ikufae. Mipangilio miwili kuu ni Shughuli kwenye Programu na Wavuti na Historia ya YouTube.
Vidhibiti hivi vikiwa vimewashwa:
- Taarifa kuhusu shughuli zako kwenye programu na tovuti za Google huhifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google na
- Taarifa zilizohifadhiwa hutumiwa kufanya hali yako ya kutumia Google ikufae
Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu
Huhifadhi shughuli zako kwenye tovuti na programu za Google, kama vile huduma ya Tafuta na Ramani na hujumuisha maelezo husika kama vile mahali. Pia inahifadhi historia kwenye Chrome na shughuli zilizosawazishwa kutoka kwenye tovuti, programu na vifaa ambavyo vinatumia huduma za Google.
Shughuli zako hutumiwa kukupa matokeo ya utafutaji kwa haraka zaidi, mapendekezo bora na hali za utumiaji zinazokufaa kwenye Ramani za Google, Tafuta na Google na huduma nyinginezo za Google.
Historia ya YouTube
Huhifadhi video unazotazama na mambo unayoyatafuta unapotumia YouTube.
Historia yako ya YouTube hutumiwa kufanya hali ya utumiaji wako wa YouTube na programu zingine ikufae, kama vile matokeo yako ya utafutaji.
Ninawezaje kufuta data ya Shughuli Zangu?
Unaweza kufuta data iliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google. Data unayoamua kufuta kabisa huondolewa kwenye mifumo yetu. Tunafuata mchakato makinifu wa kuhakikisha kwamba data hii imeondolewa kabisa kwenye seva zetu au imehifadhiwa kwa njia ambayo haiwezi kuhusishwa nawe.
Tembelea Shughuli Zangu ili ukague shughuli zilizohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google, kama vile vitu ulivyotafuta, ulivyosoma na kutazama. Unaweza kufuta baadhi ya shughuli zako au shughuli zako zote katika kipindi mahususi cha muda.
Unaweza pia kuchagua shughuli zako zifutwe kiotomatiki.
Ninawezaje kupakua maudhui yangu?
Maudhui yako ni pamoja na vitu kama vile barua pepe, picha, video, hati, majedwali, maoni, anwani na matukio ya kalenda.
Tembelea sehemu ya Pakua data yako ili uweke kumbukumbu ya maudhui yako — ili uyahifadhie nakala au uyapeleke kwenye kampuni nyingine iwapo ungependa kujaribu huduma tofauti.
Ninapata vidhibiti gani nikiwa nimeondoka kwenye akaunti?
Una vidhibiti vinavyokuwezesha kuchagua jinsi ya kutumia Google, hata ukiwa umeondoka kwenye akaunti. Ukiwa umeondoka kwenye akaunti, tembelea g.co/privacytools ili ubadilishe mipangilio hii:
Kubadilisha utafutaji ukufae
Hutumia utafutaji wako kwenye Google kutoka kwenye kivinjari hiki ili kukupa matokeo na mapendekezo yanayokufaa zaidi.
Historia ya Mambo Uliyotafuta na Video Ulizotazama kwenye YouTube
Hutumia shughuli zako kwenye YouTube, kama vile video unazotazama na mambo unayotafuta, kufanya YouTube ikufae.
Unaweza pia kuzuia baadhi au vidakuzi vyote katika kivinjari chako, lakini hatua hii inaweza kusababisha vipengele fulani kwenye wavuti viache kufanya kazi. Kwa mfano, tovuti nyingi huhitaji vidakuzi viwashwe unapotaka kuingia katika akaunti.
Watumiaji walioondoka kwenye akaunti wanaweza pia kuchagua iwapo wangependa kuona matangazo yaliyowekwa mapendeleo, ijapokuwa hatuweki mapendeleo ya matangazo kwa watu wenye umri fulani.