Hili ni toleo la awali la Sera yetu ya Faragha. Toleo la sasa la Sera yetu ya Faragha linapatikana hapa.
"matokeo muhimu zaidi ya utafutaji"
Mifano
- Kwa mfano, tunaweza kufanya utafutaji kuwa wa maana zaidi na wa kupendeza kwako kwa kujumuisha picha, machapisho na zaidi kutoka kwako na marafiki wako. Ukiwa umeingia kwa kutumia Google+, utapata matokeo yanayokufaa na wasifu wa watu unaowajua au kufuata na watu wanaokujua au kukufuata wanaweza kuona machapisho na wasifu wako katika matokeo yao. Unaweza kubadilisha mipangilio ya wasifu wako wakati wowote ikiwa hutaki Google na injini zingine za utafutaji kuorodhesha wasifu wako. Pata maelezo zaidi.
- Wakati umeingia kwenye Akaunti yako ya Google na umewasha Historia ya Wavuti, unaweza kupata matokeo muhimu zaidi ya utafutaji kulingana na Historia yako ya Wavuti. Historia ya Wavuti inajumuisha utafutaji wako na shughuli zingine za wavuti. Matokeo yako ya utafutaji pia yanaweza kugeuzwa kukufaa kwa kutumia shughuli yako ya utafutaji kutoka kwa kompyuta yako hata ikiwa umeondoka kwenye akaunti. Pata maelezo zaidi.