Hili ni toleo la awali la Sera yetu ya Faragha. Toleo la sasa la Sera yetu ya Faragha linapatikana hapa.
"huenda ikakusanya na kuchakata maelezo kuhusu eneo lako halisi"
Mifano
- Kwa mfano, Ramani za Google zinaweza kuweka mwonekano wa ramani kwenye eneo lako la sasa. Pata maelezo zaidi. Ikiwa unatumia Ramani za Google kwa simu ya mkononi, tunatumia GPS, WiFi na mawimbi ya mnara wa vifaa vya mkononi ili kuamua eneo lako. Pata maelezo zaidi.
- Wakati uko karibu na kituo cha basi au kituo cha treni, Google Msaidizi inaweza kukuelezea ni basi au treni zipi zitafuata.
- Historia ya Eneo inaruhusu Google kuhifadhi historia ya data yako ya eneo kutoka kwa vifaa vyote ambapo umeingia kwenye Akaunti yako ya Google na umewasha Kuripoti mahali ulipo. Data ya Historia ya Eneo na ya Kuripoti mahali ulipo inaweza kutumika na programu yoyote ya Google au huduma. Kwa mfano, Ramani za Google zinaweza kuitumia kuboresha matokeo yako ya utafutaji kulingana na maeneo ambayo umekuwa. Pata maelezo zaidi.