Hili ni toleo la awali la Sera yetu ya Faragha. Toleo la sasa la Sera yetu ya Faragha linapatikana hapa.

"unganisha maelezo ya kibinafsi kutoka kwa huduma moja na maelezo, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kibinafsi, kutoka kwa huduma zingine za Google"

Mifano

  • Kwa mfano, wakati umeingia katika Akaunti yako ya Google na utafute kwenye Google, unaweza kuona matokeo ya utafutaji kutoka kwenye wavuti ya umma, pamoja na kurasa, picha, na machapisho ya Google+ kutoka kwa marakifi wako na watu wanaokujua au wanaokufuata kwenye Google+ wanaweza kuona machapisho yako na wasifu katika matokeo yao. Unaweza pia kupata maelezo muhimu kutoka kwa maudhui uliyo nayo katika bidhaa zingine za Google ambazo unatumia kama Gmail au Google Kalenda.
  • Ikiwa unapanga safari ya Italia, na utafute "florence" kwenye Google, unaweza kuona picha au makala kutoka kwa marafiki wako kuhusu Florence katika matokeo yako ya utafutaji. Matokeo haya huifanya iwe rahisi kuchunguza mapendekezo yao na kuanza mazungumzo kuhusu maeneo yapi ya kuona. Pata maelezo zaidi.
  • Google Msaidizi hutumia data ambayo huenda umehifadhi katika bidhaa zingine za Google. Kwa mfano, ikiwa una utafutaji uliohifadhiwa katika Historia yako ya Wavuti, Google Msaidizi inaweza kuonyesha kadi za maelezo kulingana na alama za michezo, hali ya ndege, na kadhalika, kulingana na utafutaji huo wa awali. Ili kusimamia Historia yako ya Wavuti, tembelea google.com/history/. Unaweza kufuta au kusimamisha Historia yako ya Wavuti na bado utumie Google Msaidizi, lakini aina fulani ya maelezo haitonekana. Pata maelezo zaidi.
  • Ikiwa una ingizo la Google Kalenda la miadi ya biashara, Google Msaidizi inaweza kuangalia trafiki na ipendekeze wakati wa kuondoka ili kufika miadi yako kwa wakati.
Programu za Google
Menyu kuu