Google News ni kijumlishaji cha habari zinazolingana na mapendeleo yako, ambacho hupanga na kuangazia kile kinachotokea ulimwenguni ili uweze kugundua zaidi taarifa ambazo ni muhimu kwako.
Ukiwa na Google News, utapata:
MUHTASARI WAKO: Huenda ikawa vigumu kufuatilia kila taarifa muhimu kwako, hivyo Muhtasari Wako hurahisisha kuendelea kufahamu kuhusu mambo muhimu kwako na yale yanayokuhusu. Hujisasisha siku nzima ili ikuletee vichwa vikuu vya habari za mahali unapoishi, za kitaifa na za kimataifa, pamoja na habari zinazokulenga binafsi kulingana na mambo yanayokuvutia.
HABARI ZA MAHALI UNAPOISHI: Fahamu zaidi kuhusu jumuiya yako kupitia taarifa na makala kutoka katika vyombo vya habari vya eneo unapoishi. Weka mapendeleo na uchague maeneo mengi ili uweze kujua kinachoendelea karibu nawe au mahali popote unapoishi.
HABARI KWA KINA: Fuatilia kwa kina zaidi taarifa yenye mitazamo mbalimbali. Kipengele cha Habari kwa Kina hupangilia kila kitu mtandaoni kuhusu taarifa, huku kikionyesha na kuangazia habari kutoka katika vyanzo na vyombo tofauti. Kwa kugusa tu, utagundua mwelekeo wa taarifa na jinsi kila mtu anavyoiripoti.
TAARIFA KWA AJILI YAKO: Sehemu ya Kwa Ajili Yako hutoa habari zinazolingana na mapendeleo yako kulingana na mambo yanayokuvutia. Dhibiti na uweke mapendeleo ya makala unazoziona kulingana na mada na vyanzo unavyovipenda.
FIKIA UKITUMIA KIFAA CHOCHOTE: Google News imeundwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wenye simu za aina tofauti na viwango tofauti vya muunganisho. Wakati muunganisho wako haupo thabiti au unahitaji kuokoa data, Google News itaendelea kufanya kazi bila shida kwa kupunguza ukubwa wa picha na kupakua data kidogo. Makala yanaweza kupakuliwa kupitia Wi-Fi na kuhifadhiwa ili uyasome baadaye ukiwa nje ya mtandao.
Je, unapendelea kupata habari zako kwenye Kompyuta ya kupakata au Kompyuta ya mezani? Oanisha programu ya vifaa vya mkononi ya Google News na tovuti yetu ya Kompyuta ya mezani, news.google.com, ili uweze kupata na kufikia habari bila kujali unatumia kifaa gani.
Ilisasishwa tarehe
20 Nov 2024