Google Chrome ni kivinjari cha wavuti cha haraka, rahisi kutumia na salama. Kivinjari cha Chrome kilichotengenezwa ili kitumiwe kwenye Android, hukuletea makala ya habari zinazolingana na mapendeleo yako, viungo vya kukuwezesha kufikia tovuti uzipendazo kwa haraka na vipakuliwa. Huduma za Tafuta na Google na Google Tafsiri zimejumuishwa ndani. Ipakue sasa ili ufurahie matumizi sawa ya kivinjari cha wavuti unachopenda kwenye vifaa vyako vyote.
Vinjari haraka na uandike kidogo. Chagua kwenye matokeo ya utafutaji yanayokufaa ambayo yanaonekana moja kwa moja unapoandika na vinjari kwa haraka kurasa za wavuti ulizotembelea hapo awali. Jaza fomu za Google kwa haraka kwa kutumia kipengele cha Kujaza kiotomatiki.
Kuvinjari katika Hali Fiche. Tumia Hali Fiche ili uvinjari intaneti bila kuhifadhi historia yako ya kuvinjari. Vinjari kwa faragha kwenye vifaa vyako vyote.
Sawazisha Chrome kwenye Vifaa Vyote. Ukiingia kwenye Chrome, alamisho, manenosiri na mipangilio yako itasawazishwa kiotomatiki kwenye vifaa vyako vyote. Unaweza kufikia maelezo yako yote vizuri kwenye simu, kompyuta kibao au kompyuta yako ndogo.
Unaweza kupata maudhui yote uyapendayo kwa kugusa tu. Chrome haikuwezeshi tu kutafuta kwa haraka kwenye Huduma ya Tafuta na Google, bali imeundwa ili ikuwezeshe kupata maudhui yote uyapendayo kwa kugusa tu. Unaweza kugusa tovuti ya habari uzipendazo au mitandao ya jamii kwenye ukurasa wa kichupo kipya. Chrome pia ina kipengele cha “Gusa ili Utafute”- kwenye kurasa nyingi za wavuti. Unaweza kugusa neno au sentensi yoyote ili uanze kutafuta kwenye Google ukiwa bado kwenye ukurasa unaotumia.
Linda simu yako kwa kutumia kipengele cha Kuvinjari Salama na Google. Kipengele hiki cha Kuvinjari Salama na Google kimejumuishwa katika Chrome. Kipengele hiki huimarisha usalama wa simu yako kwa kukuonyesha onyo unapojaribu kuingia kwenye tovuti au kupakua faili hatari.
Pakua kwa haraka na uangalie kurasa za wavuti na video nje ya mtandao Chrome ina kitufe maalum cha kupakua, hivyo unaweza kupakua video, picha na kurasa nzima za wavuti kwa urahisi kwa kugonga mara moja tu. Chrome pia imejumuisha ukurasa wa mwanzo wa vipakuliwa, ambapo unaweza kufikia maudhui yote uliyopakua, hata ukiwa nje ya mtandao.
Huduma ya Tafuta na Google kwa Kutamka. Chrome ni kivinjari halisi cha wavuti unachoweza kuzungumza nacho. Tumia sauti yako ili upate majibu popote ulipo bila kuandika na bila kutumia mikono. Unaweza kuvinjari na kusogeza haraka zaidi kwa kutumia sauti yako mahali popote, wakati wowote.
Programu ya Google Tafsiri iliyojumuishwa: Tafsiri kurasa nzima za wavuti kwa haraka. Chrome ina programu ya Google Tafsiri iliyojumuishwa ili kukusaidia kutafsiri tovuti nzima kwa lugha yako kwa kugusa mara moja.
Mapendekezo mahiri yaliboreshwa zaidi. Chrome inakupa huduma inayokufaa kwa mambo unayopenda. Kwenye ukurasa wa kichupo kipya, utapata makala yaliyochaguliwa na Chrome kulingana na mambo uliyovinjari awali.
Ilisasishwa tarehe
21 Nov 2024